Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi Amchimba Mkwara Makambo

Makambo Heritier Hat Trick Nabi Amchimba Mkwara Makambo

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewaonya wachezaji wa timu hiyo akiwemo mshambuliaji wake, Heritier Makambo kwa kumwambia kuwa asifikirie kama kuna mchezaji mkubwa kwake kikosi chake licha ya kufunga mabao matatu kwenye mchezo wa Kombe la FA.

Nabi ametoa kauli hiyo kufuatia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa Kombe la FA waliocheza juzi Jumatano dhidi ya Ihefu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Makambo amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza ndani ya timu hiyo kabla ya juzi kupewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambapo alifanikiwa kufunga ‘hat trick’ katika ushindi wa mabao 4-0.

Nabi alisema kuwa licha ya mshambuliaji huyo kufunga hat trick katika mchezo huo lakini anapaswa kutambua kuwa haiwezi kuwa kigezo cha kumpa nafasi ya upendeleo kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwa hakuna mchezaji mkubwa kwake zaidi ya timu yenyewe.

“Nadhani amefanya kitu kikubwa lakini sitegemi kwamba ndiyo itapelekea kutoa nafasi kubwa ya upendelo upande wake kwa sababu wachezaji wote kwenye timu yangu wapo katika daraja moja, hakuna mchezaji mkubwa kwamba huyu anawazidi wenzake.

“Kiukweli nimeweka hivyo wachezaji wangu na kila mchezaji atacheza kwa nafasi yake ambayo itakuwa imepatikana lakini siyo kwa sababu ya ukubwa wa majina yake, kwangu Yanga ndiyo kubwa na siyo wachezaji isipokuwa wapo hapa kwa ajili ya kuipigania Yanga iendelee kubaki kuwa kubwa na siyo wao,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live