Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Na leo tena

Skysports Ivan Toney Brentford 6054722 Arsenal wamekuwa na matokeo yasyo ya kurudhisha michezo ya hivi karibuni

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Haijaisha, hadi iishe kabisa. Kinyonge Arsenal iliporomoshwa kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England usiku wa Jumatano iliyopita, lakini jioni ya leo Jumamosi ina fursa ya kurejea kukamatia usukani wa ligi hiyo na kuamsha moto wa kusaka ubingwa.

Kuanzia saa 9:30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, Arsenal itakuwa na jambo lake huko Villa Park wakati itakapokwenda kukabilisha na Aston Villa katika mchakamchaka huo wa Ligi Kuu England, ikisaka pointi tatu za kuiweka kileleni kibabe.

Lakini, utamu wa mechi hiyo ni kwamba Kocha Mikel Arteta atakwenda kumenyana na yule aliyempisha Emirates, Unai Emery. Nani atatoboa? Aston Villa na Arsenal kwenye Ligi Kuu England zimekutana mara 55, mechi 14 zilimalizika kwa sare, huku Aston Villa ikishinda 11 na Arsenal 30. Katika mechi 11 ilizoshinda Aston Villa, tano zilikuwa kwenye Uwanja wa Villa Park na sita ugenini, huku Arsenal 17 imeshinda nyumbani na mara 13 iliibuka na ushindi ugenini kwa Aston Villa.

Takwimu hizo zinaiweka pazuri Arsenal kwenye uwezekano mkubwa wa kushinda, huku katika mechi zao tano za mwisho kukutana, The Gunners imeshinda tatu za mwisho na Aston Villa ilishinda mbili za mwanzo. Rekodi cha kila mmoja kwenye mechi zao tatu za mwisho, Arsenal imechapwa mbili na kutoka sare moja, huku Aston Villa ikishinda moja na kuchapwa mbili – hivyo Arsenal imevuna pointi moja na Aston Villa imevuna nne kwa rekodi za mechi tatu za mwisho. Lakini, kipute cha leo Arsenal kazi ni moja tu, kurudi kileleni.

Hata hivyo, Arsenal kileleni inaweza kukaa kwa muda tu kama itashinda au kutoka sare dhidi ya Aston Villa, endapo kama wabaya wao Manchester City nao watapata matokeo mengine yasiyokuwa ya kichapo dhidi ya Nottingham Forest huko City Ground saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Man City, ambayo kwa sasa ipo kileleni imelingana pointi na Arsenal, 51 kila moja, hivyo kila moja itahitaji ushindi katika mechi za leo ili kuendelea na vita hiyo ya vuta nikuvute kileleni kwenye msimamo wa ligi. Kwa Man City na Arsenal kwa siku ya leo, atakayepigwa tu imekula kwake jumla. Arsenal itakuwa bado ina mchezo mmoja mkononi.

Nottingham Forest si wanyonge kwa Man City, kwenye mechi saba walizokutana kwenye Ligi Kuu England kila moja imeshinda mara mbili huku mechi tatu zilimalizika kwa sare. Forest imeshinda nyumbani, wakati Man City imegawa nyumbani na ugenini.

Mechi nyingine za mikikimikiki hiyo, Brentford itakuwa nyumbani kukipiga na Crystal Palace katika mechi ya kibabe, huku Brighton nayo ikimwaga nyumbani kumalizana na Fulham. Chelsea itakuwa Stamford Bridge kujaribu kusaka ushindi muhimu mbele ya Southampton huku Everton itakuwa Goodison Park kuikaribisha Leeds United na Wolves itashuka dimbani kukipiga na Bournemouth. Shughuli pevu nyingine kwenye ligi hiyo itakuwa usiku wa saa 2:30 kwa saa za Afrika Mashariki, wakati Newcastle United inayong’ang’ana isitoke kwenye Top Four itakapokuwa nyumbani St James’ Park kucheza na Liverpool.

Newcastle United na Liverpool kwenye Ligi Kuu England zimekutana mara 55, na zilitoka sare kwenye mechi 12, huku Newcastle unishinda 11 na Liverpool 32. Kwenye mechi ilizoshinda Newcastle 10 ilikuwa nyumbani na moja ugenini, wakati Liverpool ilishinda 22 uwanjani Anfield na 10 St James’ Park. Kazi ipo.

Kesho, Jumapili kutakuwa na mechi mbili tu kwenye ligi hiyo, ambapo Manchester United itahitaji kuongeza presha kwa timu mbili ziliopo kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo, wakati itakapokuwa uwanjani Old Trafford kukipiga na Leicester City. Man United imezidiwa pointi tano na timu zilizopo kileleni, hivyo ushindi dhidi ya chama hilo la Brendan Rodgers utazidi kuiweka kwenye vita ya kuwania taji. Man United na Lei cester City zimekutana mara 33 kwenye Ligi Kuu England na tisa zilimalizika kwa sare, huku Lei cester ikishinda nne tu, mbili nyumbani na mbili ugenini, huku M an Un ited ikish inda 20, mara 10 nyumbani na 10 nyingine ugenini. Kwenye mechi tano zilizopita baina yao, Leicester City imeshinda mbili, Man United moja na mbili sare.

Hakika Ligi Kuu England wikiendi hii patachimbika. Mchezo mwingine wa mwisho utakuwa wa London derby, wakati Tottenham itakapokipiga na West Ham United.

Chanzo: Mwanaspoti