Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB yawapa darasa wanamichezo BAMATA

NMB BAMATA NMB yawapa darasa wanamichezo BAMATA

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Meneja wa kanda ya ya kusini wa benki ya NMB Janeth Shango katika mashindano ya baraza la majeshi Tanzania (BAMATA) alisema kuwa pamoja na udhamini huo wametoa elimu ya kuweka akiba.

“Katika michezo hii tutapata fursa ya kutoa elimu mbalimbali ya kifedha namna bora ya kutunza akaunti na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki yetu ambapo zitasaidia katika uwekaji wa akiba”

“Tunaenda kutoa elimu kuhusiana na akaunti ambapo zipo za kupitisha miamala na akaunti za akiba na tutaongelea kupitia akaunti zetu mbalimbali lakin zipo za akiba ambazo mfanyakazi anaweza kutumia nafasi hiyo kujiwekewa akiba lakini pia kama kuna vikundi”

“Hawa wafanyakaazi wanapokea mishahara na kuutmia lazima mtu awekeze ambapo ipo akaunti ya wekeza mwekezaji anaweza kuwekeza kuanzia miaka 6-20 hii ni ya muda mrefu zaidi hii huduma kwa wanajeshi pia ipo ya muda mfupi yaani unaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu hadi miaka 2 katika kipindi hicho tunataoa elimu ya bima wanajeshi ni kama wafanyakazi wengine wanahitaji kupata faraja pale wanapopata majanga”

“Tunaenda kuelezea aina za mikopo ambapo wao wanapata mishahara wanaweza kukopa kupitia mshahara wao sio kukupa unaenda kununua gari tunayo mikopo ya magari boda na nyumba ambayo unpata kwa wakati na mapema zaidi”

Chanzo: Mwanaspoti