Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NGAOYAJAMII2022: Kuwaona Simba, Yanga buku tano tu

Ngao Ya Jamii Agosti Kuwaona Simba, Yanga buku tano tu

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Limetangaza viingilio vya mchezo wa Ngao ya Jamii kuelekea ufunguzi wa msimu mpya 2022/2022.

Mchezo huo unavikutanisha vilabu vikongwe nchini na wapinzani wa Jadi Simba na Yanga.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii utapigwa Agosti 13 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kumbu kumbu zinaonesha mchezo huo kwa mwaka uliopita uliwakutanisha watani hao na Yanga wakaibuka kinara kwa bao la pekee lililowekwa wavuni na Fiston Mayele.

Viingilio katika mchezo huo, ni vya aina tano ambavyo ni kama vifuatavyo;

VIP A- 30,000

VIP B- 20,000

VIP C- 15,000

Viti vya Rangi Machungwa - 7000

Viti vya Bluu & Viti vya Kijani - 5000

Chanzo: www.tanzaniaweb.live