Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBCPL: Simba kuanza mzunguko wa pili na Tanzania Prisons keshokutwa

NBCPL: Simba Kuanza Mzunguko Wa Pili Na Tanzania Prisons Keshokutwa NBCPL: Simba kuanza mzunguko wa pili na Tanzania Prisons keshokutwa

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumalizana na mfupa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Wekundu wa Msimbazi Simba SC wanarejea kwenye Ligi Kuu ya NBC na bila kupoteza muda kesho kutwa wanawakaribisha Tanzania Prisons.

Simba walifunga mzunguko wa kwanza wakiwa na alama 36, na mpaka sasa msimamo unaonesha wapo nafasi ya tatu na alama hizo. Juu yao yupo Azam FC na Yanga SC waliolingana alama 43.

Azam yeye ammemzidi Yanga kwa kucheza michezo 19 huku Yanga akiwa amecheza michezo 16 na Simba akiwa amechezamichezo 15.

Kwa upande wa Tanzania Prisons, wao wapo nafasi ya sita kwenye msimamo wakiwa na alama zao 24. Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba ilimfunga Tanzania Prisons 3-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live