Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIUPDATES: Mshery asimama langoni dhidi ya Dodoma

FH3a7kWXIAMujBP Abuutwalib Mshery

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango mpya wa Yanga, Abuutwalib Mshery ameanza kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji inayochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mshery alisajiiwa Jumatano Desemba 29,2021 na kufanya mazoezi siku mbili tu na timu hiyo na leo amepewa jukumu la kuiongoza Yanga.

Kinachombeba Mshery kuanza kwenye mchezo huu dhidi ya makipa wenzake ni utimamu wa mwili (Match Fitness) ambayo Eric Johola hana.

Mshery alikuwa kipa namba moja kwenye kikosi cha Mtibwa huku mchezo wake wa mwisho kucheza ni Jumanne dhidi ya Coastal Union.

Wakati huo huo kiungo mpya, Salum Abubakari ‘Sure Boy’ yeye ameanzia benchi kwenye mchezo huo.

Kikosi kinachoanza ni Abuutwalib Mshery, Dickson Job, Yassin Mustapha, Yanick Bangala, Bakari Mwamnyeto na Zawadi Mauya.

Wengine ni Khalid Aucho, Jesus Moloko, Saido Ntibazonkiza,Feisal Salum na Fiston Mayele. Benchi ni Eric Johola, David Bryson, Paul Godfrey, Mukoko Tonombe, Salum Abubakari, Deusa Kaseke, Dickson Ambundo, Farid Mussa na Heritier Makambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live