Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIUPDATES: Hivi hapa vikosi vinavyoanza mchezo wa leo Simba vs Yanga

Simba Yanga Makipa Vikosi vinavyoanza mchezo wa leo

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo wa Kariakoo Simba na Yanga wanahesabu dakika tu kuja kupimana ubavu mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo huo unaovuta hisia za wengi unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa hasa ikizingatiwa timu hizo zinalingana alama wote wakiwa na alama 18 Yanga wakikamata nafasi ya pili na Simba wakikamata nafasi ya tatu.

Ushindi katika mchezo wa leo utamfanya mshindi kwenda kuongoza jedwali la msimamo wa Ligi ambalo kwa sasa Azam ndio kinara wakiwa na alama zao 19.

Yanga watahitaji kulipa kisasi baada ya kupoteza mchezo wao wa mwisho walipokutana kwenye Ligi baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-0, magoli ya Inonga Baka na Kibu Denis.

Hivi hapa vikosi vya Timu zote mbili vinavyoanza mchezo wa leo;

Simba SC:

Manula

Kapombe

Zimbwe Jr

Che Malone

Inonga

Kanoute

Ngoma

Chama

Kibu D

Saido

Baleke

Yanga SC:

Diarra

Yao

Lomalisa

Bacca

Job

Aucho

Mudathir

Maxi

Pacome

Aziz Ki

Musonda

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: