Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIUPDATES: Hiki hapa kikosi cha Yanga kinachoanza vs Geita Gold

Yanga Warm Up Mbarali.jpeg Wachezaji wa Yanga wakipasha misuli

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku tatu tu tangu itoke kupoteza mechi ya kwanza katika Ligi Kuu kwa msimu huu, Yanga leo jioni itashuka tena ugenini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, kuvaana na Geita Gold, huku rekodi zikiibeba dhidi ya wenyeji wao hao waliotoka kupasuka kwenye michezo miwili iliyopita ya ligi hiyo.

Yanga ina kila sababu ya kusaka ushindi ili kuwapa ari ya kuhakikisha inapata matokeo ya ushindi yatakayofanya ifikishe pointi 12 na kuzidi kuipa presha Simba na Azam zinazokimbizana nazo juu katika msimamo wa Ligi.

Sababu ya pili kwa Yanga kutaka ushindi ni kuwapooza machungu mashabiki wa timu hiyo baada ya kipigo cha mechi iliyopita mbele ya Ihefu SC ilipolala mabao 2-1, matokeo ambayo yaliwaondoa kileleni.

Hiki hapa kikosi cha Yanga kinachoanza mchezo wa leo;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: