Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIUPDATES: Half Time, Ngoma ngumu kwa Mkapa

Simba Vs Dodoma Simba 0 - Dodoma Jiji 0

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dakika 45 za Kipindi cha kwanza zinakamilika katika Uwanja wa Kumbu Kumbu ya Benjamin Mkapa, sio simba mwenyeji wala Dodoma Jiji aliefanikiwa kuona lango la mwenzake.

Simba wanaonekana kucheza kwa presha ya hali ya juu na kujikuta wanapoteza mipira mara kwa mara.

Dodoma Jiji wanonekana kuwa wagumu huku wakiwa na idadi kubwa ya wakabaji katika eneo lao la mwisho wakihakikisha wanajilinda vyema na kutoruhusu bao.

Mpira una kasi ya hali ya juu huku Dodoma Jiji wakicheza faulo za mara kwa mara ili kupunguza kasi ya mashambulizi katika upende wao.

Seif Karia anaonekana kufanya vizuri kwa dakika 45 za Kipindi cha Kwanza, akifanya kazi nzuri kwa Dodoma Jiji.

Tusubiri kuona ni namna gani walimu watabadili mbinu ili kuweza kuondoka na alama tatu katika mchezo wa leo.

John Rafael Bocco amekwenda nje baada ya kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake imechukuliwa na Meddie Kagere.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live