Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIUPDATES: Half Time, Banda aitanguliza Simba kwa Mkapa

Banda Peter Banda akiifungia Simba goli la kuongoza kipindi cha kwanza

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usajili mpya umelipa. Ndivyo watoto wa mjini wanavyoweza kusema baada ya Winga aliesajiliwa msimu huu Peter Banda kuifungia Simba SC goli la uongozi kwa Mkapa Dar es Salaam.

Banda ameifungia Simba goli lake la kwanza msimu huu tangu aliposajiliwa dirisha lililopita, na alianza kwa kusua sua sana ndani ya kikosi hicho.

Goli la Simba limefungwa mnamo dakika ya tisa ya mchezo, baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Kibu Denis ambe nae ni miongoni mwa usajili mpya ndani ya kikosi cha Simba.

Nahodha John Bocco amekosa nafasi ya wazi katika dakika 45 za kwanza baada ya kushindwa kumalizia pasi safi ya Banda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live