Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIREVIEW: Tazama magoli yote, Simba vs Geita Gold (+Video)

Video Archive
Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya wenyeji, Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Disemba 18, Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji na Nahodha, John Bocco dakika ya 12 na viungo Mzambia Clatous Chama dakika ya 40, Msenegal Pape Ousmane Sakho mawili dakika ya 47 na 75 na Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kibu Dennis Prosper dakika ya 89.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 16 na kurejea nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja Azam FC baada ya wote kucheza mechi 16, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 22 za mechi 16 nafasi ya saba.

Na wanaoongoza Ligi Kuu ni mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 41 za mechi 16 pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live