Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIREVIEW: Tazama magoli yote, Simba vs Dodoma Jiji (+Video)

Video Archive
Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao pekee la mshambuliaji mpya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean Toria Baleke Othos limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Baleke aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya kwao, Lubumbashi baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo pia Nejmeh SC ya Lebanon alifunga bao hilo dakika ya 45 na ushei akitumia makosa ya kipa wa Dodoma Jiji na walinzi wake.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.

Kwa upande wao Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 21 za mechi 21 sasa nafasi ya 12.

Tanzaniaweb tunakusogezea matukio yote muhimu katika mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live