Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIREVIEW: Tazama magoli yote Ligi Kuu Disemba 17 (+Video)

NBC PREVIEW Mchezo wa Dodoma Jiji vs Polisi Tanzania uliisha kwa sre ya 1-1

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Disemba 17, Ligi Kuu Bara maarufu kama NBC Primia ligi msimu wa 2021/2022 iliingia katik raundi ya tisa, ambapo michezo mitatu ilipigwa.

Sasa TanzaniaWeb inakuletea uchambuzi na matukio yote muhimu katika michezo hiyo iliyopigwa Ijumaa ya Disemba 17.

Fuatilia hapa chini kuona video za magoli yote, wafungaji na nafasi ya kila timu katika msimamo wa Ligi.

GEITA GOLD VS RUVU SHOOTING

Huu ulikuwa ni mchezo wa awali kabisa uliopigwa katika dimba la Nyankumbu Mkoani Geita na kushuhudia maafande wa Ruvu Shooting wakiondoka vichwa chini kwa goli la dakika za lala salama lililofungwa na Mpole.

Mchezo huu ulimalizika kwa Geita Gold kuibuka na ushindi wa magili 2-1, ushindi ambao umewapeleka mpaka nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama zao 8.

Tazama magoli yalivyofungwa katika mchezo huo;







MBEYA KWANZA VS NAMUNGO

Mchezo ulipigwa katika dimba la Kumbu kumbu ya Sokoine kule Jijini Mbeya, na kushuhudia jinamizi la matokeo mabovu likiendelea kuwaandama wageni hao katika Ligi Kuu.

Mbeya Kwanza walikubali kichapo cha goli 1-0, Goli lililofungwa na Lusajo kipindi cha kwanza.

Ushindi huo umewapeleka Namungo mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi na kuwaacha Mbeya kwanza katika hatari ya kushuka daraja.

Tazama hapa Goli la Namungo;

DODOMA JIJI vs POLISI TANZANIA

Mchezo huu uliopigwa majira ya saa 1:00 ulishuhudia ukimalizika kwa sare ya magoli 1-1.

Kwa sare hii Polisi Tanzania wanaendelea kubaki nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama zao 15, huku Dodoma Jiji wakiwa nafasi ya tano.

Tazama magoli yote yalivyofungwa kwenye mchezo huo;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live