Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBC yaingia Mkataba wa miaka mitatu kuidhamini Ligi kuu Bara

FBAJGjbVEAUH4RF Logo mpya itakayotumika baada ya NBC kudhamini Ligi kuu

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kuidhamini Ligi kuu Tanzania Bara.

Mkataba huo ni wa miaka mitatu (3) na kwa kuanza Benki ya NBC imetoa kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni 2.5 kabla ya VAT kwa msimu wa 2021/2022.

Ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2022 pazia lake lilifunguliwa Septemba 27 na mpaka inakamilika mizunguko miwili ya Ligi hiyo bado hakukuwa na mdhammini (Tittle Sponsor) Ligi hiyo kwa sasa itatambulika kama NBC Premier League (Ligi Kuu ya NBC)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live