Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBA All Stars 2022 babu kubwa, Curry balaa!

STEPH Stephen Curry akiwa ameshikilia tuzo yake ya KIA NBA MVP All Stars 2022

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Timu ya Lebron James imefanikiwa kuibuka na ushindi wa alama 163-160 dhidi ya timu ya Kevin Durant kwenye mchezo wa fainali wa Kobe Bryant NBA All Stars alfajiri ya leo Jumatatu Februari 21, 2022 Cleveland, Nchini Marekani.

Stephen Curry wa Golden State Warriors ambaye alfajiri ya leo ameichezea timu Lebron James ameibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo huo na kupewa tuzo ya ‘KIA MVP NBA All Stars 2022’ kufuatia kiwango bora alichoonesha.

Curry pia ameweka rekodi ya kuwa mchezji pekee kufunga ‘3-pointers’ 16 na alama 50 zikiwa ni nyingi zaidi kwenye historia ya michezo hiyo tokea kuanzishwa kwake.

Timu ya Lebron ilikuwa na nyota kama vile, Giannis Antetokounmpo (Milwaukee Bucks), Demar Derozan (Chicago Bulls), Stephen Curry (Golden State Warriors) na Nikola Jokic  (Denver Nuggets).

Kwa upande wa timu ya Kevin Durant kulikuwa na nyota kama Ja Morant (Memphis Grezzlies), Trae Young (Atlanta Hawks), Joel Embiid (Philadelphia 76ers), Zach Lavine (Miami Heats) na Luka Doncic (Dallas Mavericks).

Kumbuka mchezo wa fainali ya Kobe Bryant NBA All Stars ni michezo ambayo NBA huwapa nafasi mashabiki kuwapigia kura wacheza wachache ambao wamefanya bora zaidi ili kucheza mchezo wa fainali wenyewe kwa wenyewe kila msimu.

Chanzo: eatv.tv