Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

N'golo Kante, Reece James hatarini kulokosa Kombe la Dunia

Golo Kante , Reece James N'golo Kante na Reece James mazoezini

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Klabu ya Chelsea ya England kiungo mkabaji Ngolo Kante pamoja na mlinzi wa kulia Reece James huenda wakakosa michuano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar kutokana na kuandamwa na majeruhi.

Kocha Mkuu wa klabu hiyo Graham Potter amethibitisha taarifa za Ngolo Kante kupata majeraha mapya wakati akifanya mazoezi na klabu yake ikiwa ni siku chavhe baada ya kurudi mazoezini akitoka kuuguza majeraha ya muda mrefu.

Kante na Reece James wote kwa pamoja wnaatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa klipindi kisichopungua miezi miwili licha ya kuwa Potter alibainisha kuwa wachezaji wote hao wawili wanatarajiwa kukutana na madaktari bingwa ili waweze kuona namna ya kukabiliana na majeraha yao.

Taarifa kutoka Gazeti maarufu la Habari la Ufaransa la El Equipe limeripoti kuwa Ngolo Kante hayupo kwenye orodha ya kikosi cha timu ya taifa ua Ufaransa kinachosafiri Kwenda Qatar kwa ajili ya mashindano ya fainali za Kombe la Dunia huku mitandao mbalimbali na vyombo vya Habari vya nchini Uingereza vikibainisha kuwa Reece James ana hatihati ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza chini ya Kocha Gareth Southgate.

Majeruhi haya yamekuja kama pigo kubwa kwa klabu ya Chelsea chini ya Kocha Graham Potter ambaye tangu amewasili klabuni hapo timu imeonekana kuanza kuimarika na kupata matokeo mazuri ikiwa ni sambamba na kuongoza kundi E la klabu bingwa barani Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live