Wakati wa mavuno kwa timu shiriki Ligi Kuu Bara na Championship ni mzunguko wa kwanza. Hapa timu ambazo zinafanikiwa kuanza kwa hesabu kubwa huwa zinamaliza vizuri.
Kikubwa ambacho kinawafanya wamalize vizuri ni ule mwendelezo wa kujiamini. Kushinda mchezo mmoja kunaongeza hali ya kuendelea kupambana kwa ajili ya mechi inayofuata.
Licha ya kwamba mchezo wa mpira ni maalumu kwa ajili ya makosa bado kuna nafasi ya kufanyia kazi makosa yenyewe. Kila mmoja anapenda kuona anapata matokeo chanya akiwa uwanjani.
Kwa namna yoyote picha ya kesho kwenye mzunguko wa pili inaanza kuandaliwa leo. Hivyo wachezaji wanapaswa kutambuwa kwamba jukumu lao ni kubwa.
Mechi ni ngumu na kila timu inapambambana kupata matokeo chanya. Mzunguko wa kwanza unakuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kila mchezaji anahitaji kuonyesha uwezo alionao.
Hapo ndipo inatokea timu zinakuwa kwenye kasi mbaya kuendelea kuwa kwenye mwendo huo na zile ambazo zilianza vizuri kuendelea kupata matokeo mazuri.
Muda ni sasa kwa kuwa mzunguko wa kwanza unaendelea kwa timu ambazo hazijawa na mwendo mzuri kurekebisha mapungufu yao.Ni ngumu kupata matokeo mazuri ikiwa hakutakuwa na maandalizi bora.
Makosa yaliyopatikana kwenye mechi zilizopita ni muhimu kufanyiwa kazi mapema ili kuyapunguza kwa mechi zijazo.
Sio Ligi Kuu Bara pekee bali mpaka Championship ni muhimu ushindani kuendelea kupata matokeo chanya kila wakati.