Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzungu wa Yanga atamani kucheza beki

Kaeda Wilson.jpeg Kiungo mshambuliaji wa Yanga Princess, Kaeda Wilson

Sun, 19 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Princess, Kaeda Wilson amesema anatamani kucheza hata nafasi ya beki ilimradi kuisaidia timu hiyo kwenye mechi tatu zilizosalia.

Kiungo huyo raia wa Marekani alijiunga na Yanga msimu huu akitokea kwenye akademi ya 7 Elite ya nchini kwao na tayari amefunga mabao manne kwenye mechi 15.

Yanga Princess iko nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na pointi 24 ikishinda mechi nane na kupoteza sita, lakini ndio timu iliyofungwa na timu tatu nyumbani na ugenini.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaeda alisema licha ya kutamani kufunga mabao mengi zaidi, lakini anatamani hata kucheza nafasi ya beki ili tu kuisaidia timu hiyo kusogea nafasi ilipo sasa.

Kaeda alisema kipindi hiki ambacho ligi imesimama kwa wiki tatu kupisha timu za taifa, anahakikisha anafanya mazoezi binafsi nje ya timu ili kulinda kiwango chake.

“Natamani kufunga zaidi nikipata nafasi, lakini nitafanya kile kocha anataka niwe, hata kama kucheza nafasi ya beki ili timu ipate matokeo tu kwa kuwa nbado tuna michezo mitatu imesalia ya ligi,” alisema Kaeda.

Chanzo: Mwanaspoti