Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzungu wa Simba Awafungia Kazi Mtibwa

Simba SC 1140x640 Mzungu wa Simba Awafungia Kazi Mtibwa

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba juzi kiliingia kambini tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mtibwa.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara leo Jumamosi saa kumi kamili kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Katika mchezo huo, Simba wataingia uwanjani wakiwa na hasira za kutoka kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Kocha Mkuu wa Simba, Mhispania Franco Pablo, alitoa mapumziko ya siku ya Jumanne pekee mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Mbeya.

Pablo alisema kuwa kikosi chake chote kiliingia mazoezini juzi Jumatano na kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Bunju Dar katika kuiandaa timu yake.

Aliongeza kuwa, atakuwa na siku mbili za kukamilisha maandalizi yake juzi Jumatano na jana Alhamisi, kabla ya kuelekea Turiani tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

“Ninauchukulia umuhimu mkubwa mchezo wetu huu wa ligi tutakaocheza dhidi ya Mtibwa Sugar wikiendi hii.

“Jana (juzi) wachezaji wote waliingia kambini tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Mtibwa ambao ni muhimu kwetu kupata ushindi.

“Hatutaki kupoteza mchezo huu, nimepata taarifa za mazingira ya uwanja tutakaoutumia, hivyo tutaingia katika mchezo huu kwa tahadhari kubwa,” alisema Pablo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live