Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzungu Yanga Princess aibua Sintofahamu, Kocha azungumza

Mzungu Yanga Princesss Mzungu Yanga Princess aibua Sintofahamu, Kocha azungumza

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga Princess inaendelea kujifua katika Uwanja wa Uhuru ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Ligi ya Wanawake huku mzungu akionekana anafanya nao mazoezi.

Juzi timu hiyo ilikuwa Uwanja wa Gymkhana Posta, Dar es Salaam ikiendelea na mazoezi akiwemo raia huyo wa kigeni ambaye yupo na timu hiyo kwa wiki mbili sasa.

Akizungumza jana Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Fredy Mbuna alisema hafahamu kuhusu usajili wa mchezaji huyo lakini amekabidhiwa kumsimamia .

Mbuna alisema viongozi wa timu hiyo wamemkabidhi kwake lakini hafahamu kama atasajiliwa dirisha dogo au la.

"Tupo nae inaenda wiki mbili sasa lakini sifahamu kuhusu yeye ila nimepewa na viongozi na nimeambiwa atafanya mazoezi na sisi ni kiungo mzuri sana." Amesema Mbuna

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: