Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzuka warudi kambini Yanga, Mukoko afunguka

Mzuka Pic Data Mzuka warudi kambini Yanga, Mukoko afunguka

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mastaa wa Yanga licha ya kwamba wanalalamika kimoyomoyo kwamba matizi ya Kocha Juma Mwambusi si mchezo, lakini wanayakubali kwamba yanawajenga kwenye pumzi.

Farouk Shikhalo ambaye ni kipa Mkenya, alisema kama kuna mashabiki wanamchukulia poa Mwambusi basi wanakosea kwani katika siku mbili tu amewachangamsha na kuwarudisha kwenye mzuka wa kazi.

Shikhalo alisema mazoezi makali katika vipindi viwili wanavyofanya sasa katika mazoezi yao yatairudishia timu yao ubora mkubwa ligi itakapoendelea.

“Tulikuwa naye kabla, wachezaji takribani wote tunamfahamu na alivyoanza binafsi naona ni kocha mzuri sana, nathubutu kusema ubora wa kikosi utarejea haraka,” alisema Shikhalo.

“Kwanza hii ratiba ya mazoezi ya mara mbili kwa siku anaonyesha ni kocha ambaye sio tu anaijua Yanga ambacho inataka bali kinachohitajika katika ushindani wa timu za ligi,” aliongeza kipa huyo wa zamani wa Bandari.

Shikhalo alisema kuwa kwa muda ambao upo sasa kabla ya kuendelea kwa ligi unaweza kumpa nafasi kubwa kocha huyo mzawa kuweza kurudisha ubora wa timu hiyo.

“Tuna siku kama 20 hapa kabla ligi haijaendelea, hiki kipindi kinaweza kumsaidia sana kurudisha ubora wa timu kwa kuwa hakuna presha ya kuingia katika mechi za mashindano,” alisema.

MSIKIE MUKOKO

Kiungo wa timu hiyo Mukoko Tonombe ambaye kesho atakwea pipa kurejea kwao DR Congo kujiunga na timu ya taifa hilo anaamini kama washambuliaji wa timu hiyo watarejesha ubora itakuwa ni hatua nzuri kwa Mwambusi.

“Shida yetu kubwa nimeona kocha ameanza kuifanyia kazi kuwa fiti lakini pia kuna shida ya kufunga, tukiweza kutumia nafasi kazi itakuwa rahisi kwa kocha na timu kwa ujumla,” alisema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz