Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzuka wa Mbrazili wa Singida FG usipime

Ricardo Ferreira Fh Mzuka wa Mbrazili wa Singida FG usipime

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Mbrazili Ricardo Ferreira ameungana na kikosi hicho huku akifurahishwa na vipaji vya nyota waliopo kutokana na ushindani.

Akizungumza baada ya kutembelea kambi iliyokuwa mjini Lindi, Ferreira alisema amefurahishwa na morali iliyoonyeshwa na mastaa huku akiahidi kutoa nafasi kwa kila mmoja.

“Nina furaha kufanya kazi na kundi kubwa la wachezaji hivyo nawaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo, kwangu ni jambo jema na naamini kwa umoja wetu tutafikia malengo ambayo viongozi kwa uwekezaji wao wanahitaji kufikia,” alisema.

Nyota wa timu hiyo, Biemes Carno alisema kocha huyo ameonyesha imani kubwa kwao huku akiweka wazi wataendelea kupambana na kutoa ushirikiano kama ilivyokuwa kwa wengine.

Ferreira amejiunga na timu hiyo baada ya Mjerumani Ernst Middendorp aliyejiunga Septemba 1 kutimka kutokana na kile kilichoelezwa kutoelewa na viongozi ambao walikuwa wakimuingilia katika majukumu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live