Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzizima Dabi shida iko pale pale

Dube Prince Vs Onyango Mzizima Dabi shida iko pale pale

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa kisasi, mchezo wa kusaka heshima pia mchezo utakuwa wa Yanga kuombea mabaya Simba itakapokutana na Azam Februari 21 Uwanja wa Mkapa katika mwendelezo wa Ligi Kuu.

Zilipokutana Uwanja wa Mkapa Oktoba 27, Azam ikiwa nyumbani ilishinda bao 1-0 la Prince Dube mchezo pekee Simba ambao amepoteza hadi sasa msimu huu.

Katika michezo 15 ya Ligi Kuu walizokutana Azam ameshinda mara mbili, mchezo mwingine alioshinda ilikua Januari 28,2017 kwa bao 1-0 huku ikipoteza michezo sita na kupata sare saba.

Wakati Simba ikiwa imepoteza mchezo mmoja hadi sasa, Azam tayari imepoteza michezo mitano na sare nne huku miwili ikichapwa na Yanga, Prisons na michezo miwili mfululizo iliyopita akichapwa mbele ya Singida kisha dhidi ya Dodoma Jiji.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa ndio timu yenye safu kali ya mabao (53), Azam nayo imeonekana kuwa moja ya timu iliyoruhusu mabao mengi kwenye ligi (23) sawa na kila mchezo mmoja kuruhusu bao.

Katika michezo 22 ya Ligi Kuu, michezo nane pekee ambayo Azam haijaruhusu bao wakati Simba katika michezo hiyo hajarujusu bao katika michezo 12.

Timu zote zimefanya mabadiliko ya benchi la ufundi, Azam ilimtimua, Abdihamid Moallin ambaye alikua kocha wa kwanza kufutwa kazi msimu huu, Agosti 29 uongozi wa Azam ulipotangaza kuachana naye na timu kuwa chini ya Daniel Cadeba na Kali Ongala.

Simba ikiachana na Zoran Maki Septemba 6, na timu kuwa chini ya Juma Mgunda kwa muda akisaidiana na Suleiman Matola lakini Januari 3 mwaka huu ikimtambulisha, Robert Oliviera ‘Robertinho’ kuwa kocha mkuu kisha Januari 19, ikamtambulisha, Ouanane Sellami kuwa kocha msaidizi pamoja na Mgunda. Beki wa zamani wa Sigara, Simba na AFC Arusha, Aziz Nyoni alisema mchezo huo asilimia kubwa ushindi unaonekana kwenda kwa Simba kutokana na mwenendo mzuri walionao kwa sasa tofauti na Azam.

“Maboresho ya wachezaji wapya kwa Simba imeonekana kuwasaidia zaidi kila mmoja kwenye nafasi yake amefanya vizuri alipopewa nafasi hasa wale wanaocheza nafasi za mbele kama vile Saido (Ntibazonkiza) ameingia vyema kwenye mfuno,” alisema Nyoni.

Muhidin Cheupe aliyetamba zaidi akiwa Yanga alisema soka muda wowote linaweza kukupa matokeo usiyotarajia na mchezo huo utakuwa na ushindani kutokana na jadi ya timu hizo tangu miaka ya nyuma.

“Azam inaweza ikapoteza mbele ya timu nyingine lakini inapokutana na Simba au Yanga hapo kuna kuwa na suala lingine kabisa na hata maandalizi yake yanakuwa tofuti kutokana na heshima na uzito wa mchezo wenyewe,” alisema Cheupe.

Katika historia ya timu hizo tangu zimeanza kukutana kwa mara ya kwanza Desemba 12, 2015 na kutoka sare ya mabao 2-2 mchezo ambao umezaa mabao mengi ni ule wa Machi 4, 2020 Simba iliposhinda 3-2.

Chanzo: Mwanaspoti