Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzize siyo mshambuliaji wa kati

Mzize Kiboko.jpeg Mzize siyo mshambuliaji wa kati

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukimtazama Clement Mzize kwa haraka haraka unaweza kusema ni mshambuliaji lakini naomba nikwambie kwa namna nilivyomsoma na namna ambavyo Kocha Gamondi anamtumia, Mzize ni playmaker na sio clinical finisher.

Mzize ni mchezaji hatari sana akitokea pembeni kuliko akisimama katikati kama straika wa mwisho.

Rejea matukio haya machache utakubaliana nami;

Assist yake kwa Maxi vs Simba

Goli lake dhidi ya Azam FC

Assist yake kwa Aziz Ki vs Dodoma

Assist yake kwa Aziz Ki vs Prisons

Assist yake kwa Guede vs Singida.

Vinara wa Assists ligi kuu 23|24:

1. Assist 9 - Kipre Junior

2. Assist 8 - Stephane Aziz Ki

3. Assist 7 - Clement Mzize

4. Assist 7 - Feisal Salum

5. Assist 7 - Yao Attohoula.

Muunganiko wa Mzize na Aziz Ki katika mechi za mwisho imekuwa superb, tazama mechi ya bao 5-1 dhidi ya Simba.

Mzize ni winger namba (11) sio Centre-striker, atakayemsoma vizuri mikimbio yake anapo-drive mpira atafunga sana magoli kupitia assists zake na rebounds.

◉ Nguvu na pace yake:

Anatengeneza spaces nyingi kwa wapinzani anapo attack, si rahisi kwa beki mmoja (1) kumzuia, wanapoenda wawili (2) au watatu (3) kumkaba wanaacha mianya nyuma ambayo wachezaji wengine wa Yanga wanaitumia kufunga magoli.

Takwimu zake za msimu 2023|2024;

Mabao 6 - Ligi kuu Tanzania Bara

Mabao 5 - CRDB Confederations Cup

Mabao 3 - CAF Champions League

Bao 1 - Ngao ya Jamii.

Assist 7 - Ligi Kuu Tanzania Bara

Assist 2 - CRDB Confederations Cup.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live