Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzize namjua, sio mkubwa - Mchambuzi

Clement Mzize X Maxi Mpia Nzengeli Mzize namjua, sio mkubwa - Mchambuzi

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa kituo cha Wasafi FM, Paul Mkai amesema wanaodai kuwa mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ni mkubwa kiumri wanakosea kwani yeye anamjua na amekulia mtaani kwao.

"Watu wengi ukiwaambia Mzize ana umri wa miaka (21) hawaamini kutokana na umbo lake kubwa, wengi hawamjui. Mimi nimemuona Mzize tangu anakua, aliishi Tanga tangu utotoni kisha baadae akahamia Iringa kwa ndugu zake.

"Mzize amesoma darasa moja na mdogo wangu wa (3) Tanga na aliwahi hadi kuendesha bodaboda. Nafurahi sana kumuona anafanikiwa akiwa Yanga SC kwani amepambana sana hadi kufika hapo alipo," amesema Paul Mkai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live