Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzize kwenye nyayo za Msuva

Clement Mzize Msuva Dczs Mzize kwenye nyayo za Msuva

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kazi ya kucheza mpira siyo rahisi kama tunapokusanyana kwenye vijiwe vyetu vya kahawa halafu tunatandaza maneno, hakuna wepesi huo hata kidogo lakini ukikutana na wale ndugu zangu unaweza ukaomba jezi kesho ucheze wewe mpira wa maneno ulivyo mwepesi.

Clement Mzize ameamua kuchagua njia sahihi amewaachia mdomo watu wazungumze yeye anaitenda kazi yake.

Hii inanikumbusha Yanga SC ile ya 2016 ambayo ndani yake ilikuwa na nyota kadhaa lakini likiwemo jina la winga teleza Simon Msuva mchezaji aliyefanyiwa sub kwa kelelee za mashabiki.

Naikumbuka derby moja ya Kariakoo pale mashabiki walipoanza zomea zomea kwa Msuva na kulazimisha atolewe huku nafasi yake ikichukuliwa na Malimi Busungu (sijui yuko wapi mchezaji yule), kisha baadae Yanga SC wanafanikiwa kuitandika Simba SC kwa ushindi wa mabao 2-0, mabao ya Amis Tambwe na Malimi Busungu mwenyewe.

Hiyo inanirudisha kipindi hiki cha Mzize ambaye naye amekuwa akipitia kasumba hiyo. Ukweli ni kwamba mashabiki wa Tanzania ambao wanaojiita wafia timu siyo wavumilivu hata kidogo wanachokitaka wao ni kila siku uwape kilekile cha jana na Leo urudie, hawataki kusubiri yaani subira kwao haivuti heri Kamwe wanachelewa.

Mtazame Clement Mzize unaona hii ni future ya kesho, umbo hata uwezo wake wakumiriki mpira, mwamba yuko vizuri sana.

Kinachotusumbua kwenye akili zetu ni kutaka wachezaji wanje ndio wafanye vizuri lakini siyo wachezaji wetu na hii yote ni kwasababu hatupendani yaani ni bora tupende vya nje lakini siyo vyetu, roho mbaya hii.

Nimalizie hivi, kwa Clement Mzize kuna kitu kikubwa kinakuja kwa Yanga SC hii muichukue lakini mwisho kabisa, tupende vya nyumbani tusiwe wachoyo kwenye kugawana maua yapo kidogo tu.

Ukimpa mtu heshima yake na kumvumilia anapopitia changamoto kadhaa wewe hupungukiwi chochote ndugu yangu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live