Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzize hana bao hata moja tangu msimu umeanza

Mzize Rteee.jpeg Clement Mzize.

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo ni magumu kwa mshambuliaji ambaye kwa sasa ndiye anapewa nafasi ya kuanza na Kocha Miguel Gamondi wa Klabu ya Yanga.

Katika mechi sita ambazo Yanga wamecheza kwenye Ligi Kuu ya NBC tangu msimu huu umeanza, Clement Mzize hajafunga hata bao moja kwenye Ligi hiyo, lakini amecheza mechi zote na kuyeyusha zaidi ya dakika 400.

Katika mechi hizo, Yanga wamefanikiwa kufunga mabao 18 na kufungwa mabao manne. Mechi za Ligi alizofunga Yanga ni ile ya bao 5-0 dhidi ya KMC, bao 5-0 dhidi ya JKT, bao 1-0 dhidi ya Namungo FC, bao 3-0 dhidi ya Gita Gold na bao 3-2 dhidi ya Azam Fc huku akifungwa mechi moja dhidi ya Ihefu kwa bao 2-1.

Washambuliaji wengine wawili wa Yanga ambao wanapewa nafasi ya kufanya vizuri ni Hafiz Konkoni raia wa Ghana ambaye hata yeye ana bao moja tu kwenye Ligi na kennedy Musonda ambaye pia ana bao moja pekee kwenye ligi.

Gamondia ameendelea kumtumia Mzize kama mshambuliaji kinara na chaguo namba moja na kuwaacha Musonda na Konkoni.

Yanga vs KMC (5-0) Magoli ya Yanga yalitoka kwa Dickson Job (dakika ya 17), Stephane Aziz Ki (dakika ya 58′), Hafidh Konkoni (dakika ya 69′), Mudhathir Yahya (dakika ya 76) na Pacome Zouzoua (dakika ya 82).

Yanga vs JKT Tanzania (5-0) Mabao yalifungwa na Aziz Ki (dakika ya 45+5), Kennedy Musonda (dakika ya 54), Kouassi Yao (dakika ya 64), Maxi Nzengeli (dakika ya 79 na 88).

Yanga vs Namungo (1-0) Bao pekee la Yanga lilifungwa lilifungwa na Mudathir Yahya dakika ya 88.

Ihefu vs Yanga (2-1) Mechi iliisha kwa Yanga kupoteza kwa kufungwa bao 2-1 wakati bao la Yanga likifungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 3.

Geita vs Yanga (0-3) Mabao yalifungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 45', Aziz Ki dakika ya 45+4' na Maxi Nzengeli dakika ya 68'.

Yanga vs Azam Fc (3-2) Aziz Ki dakika ya 9, dakika ya 69 na dakika ya 72.

Yanga vs Azam FC (2-0) Kwenye michuano ya Ngao ya Jamii Yanga ilifunga mabao 2-0 mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam FC wakati ikitopa sare ya bila kufungana dhidi ya Simba SC. Mabao yalifungwa Stephane Aziz Ki dakika ya 84 na Clement Mzize dakika ya 88.

Mzize amefanikiwa pia kufunga mabao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika mechi nne za awali ambazo Yanga imecheza na kufunga mabao 10 na kufungwa bao 1 pekee.

Mabao ambayo Mzize amefunga ni; Ngao ya Jamii alifunga bao moja mechi dhidi ya Azam FC kati ya mabao mawili ambayo Yanga ilishinda.

Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Yanga dhidi ya ASAS ya Djibouti, mchezo wa mtoano raundi ya kwanza mchezo wa pili alifunga bao moja dakika ya 67 kati ya mabao 5-0 ambayo Yanga ilifunga kwenye mchezo huo.

Yanga dhidi ya Al Merrick ya Sudan, mchezo wa mtoano raundi ya pili mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Rwanda, Mzize alifunga bao moja dakika ya 78 kati ya mabao 2-0 ambayo Yanga ilifunga kwenye mchezo huo.

Yanga dhidi ya Al Merrick ya Sudan, mchezo wa mtoano raundi ya pili mchezo wa pili uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Mzize alifunga bao pekee la Yanga dakika ya 66.

Mzize hivi karibuni alihojiwa na kusema kuwa anakitaka kiatu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu akichukua mikoba ya Mkongomani Fiston Kalala Mayele.

Kwa takwimu hizo, Yanga itafute mshambuliaji mwingine?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: