Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzimu wa Simba waitesa Geita

Bocco Head Goal Mzimu wa Simba waitesa Geita

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kupata sare ya 1-1 Jumatano hii dhidi ya Azam FC, lakini benchi la ufundi la Geita Gold bado linaendelea kuweweseka na kipigo cha mabao 5-0 ilichopewa na Simba wikiendi iliyopita na kukiri kiliwavuruga mno.

Simba iliifumua Geita mabao hayo katika mechi iliyopigwa kwenye CCM Kirumba, jijini hapa kabla ya kusafiri hadi Bukoba kuifuata Kagera Sugar na kutoka sare, huku wenyeji wao wakiipokea Azam na kutoka sare ya 1-1, kikiwa kipigo cha kwanza baada ya kucheza mechi tano mfululizo bila kupoteza.

Geita ilizibania KMC, Mtibwa Sugar, Ihefu, Mbeya City na Tanzania Prisons kabla ya kupasuka kwa Simba kwa kipigo hicho cha aibu na kikubwa zaidi kwao tangu wapande daraja, na kisha kocha msaidizi Mathias Wandiba alisema kwa sasa wameanza kurejea kwenye mstari baada ya kuvurugwa na Simba.

“Tulikuwa kwenye presha kubwa baada ya kipigo kile na hata sare ya Azam haikuwa rahisi kwani mchezo ulikuwa mgumu, japo tunashukuru sasa tumeanza kukaa vyema tena,” alisema Wandiba.

Kiungo wa timu hiyo, Kelvin Nashon alisema sare waliyoipata mbele ya Azam imeleta furaha na kupunguza presha na kuwarejesha kwenye matumaini ya kufanya vizuri katika michezo ijayo.

Chanzo: Mwanaspoti