Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mziki wa kigeni Siku ya Mwananchi

Yanga Vs Augusburg Mziki wa kigeni Siku ya Mwananchi

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa Yanga, inayoshikilia mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho kwa misimu mitatu mfululizo, imesajili beki Chadrack Boka, viungo Clatous Chama aliyekuwa Simba na Duke Abuya aliyekuwa Singida BS, huku eneo la ushambuliaji kukiwa na Prince Dube kutoka Azam FC na Jean Baleke aliyewahi kuwika na Simba.

Nyota hao wanaungana na kipa Diarra Djigui, Yao Kouassi, Khalid Aucho, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Stephane Aziz KI na Kennedy Musonda waliokuwapo msimu uliopita, hivyo kama Gamondi ataka kujibu mapigo ya Fadlu ya kushuka na nyota wa kigeni watupu, basi ni eneo la beki ya kati ndio atakuwa na mapengo kwani haitakuwa na namba nne wala tano, baada ya Gift Fred kutemwa kikosini.

Langoni Yanga itaanza kama kawaida na kipa namba moja, Djigui Diarra, beki wa kulia akiwa ni Yao, huku kushoto akisimama Boka, lakini italazimika kuwaingiza Bakar Mwamnyeto, Dickson Job au Ibrahim Bacca, kucheza beki ya kati.

Kwa eneo la kiungo Gamondi ana mashine za maana kama Aucho, Maxi, Pacome, Chama na Abuya, japo atalazimika mmoja kumuanzisha benchini ili kupata uwiano mzuri, huku katika eneo la mbele la ushambuliaji anaweza kumtumia Aziz KI na Dube, huku Baleke na Musonda kuanzia benchini au kinyume chake, kwani katika eneo hilo kama ilivyo kwa kiungo kumejaa mafundi watupu wa kumrahisishia mambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: