Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mziki wa Feitoto washtua!

86005 Pic+feitoto Mziki wa Feitoto washtua!

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nyota huyo amefunga mabao mawili ya kideoni msimu huu dhidi ya KMC katika Uwanja wa Majimaji, mjini Songea na lile alilowatungua Ruvu Shooting pale kwa Mkapa jijini Dar es Salaam, pia akifanya hivyo akiwa na Taifa Stars kwenye ushindi 3-2 mbele ya Madagascar akifunga la ushindi.

Kocha wa Rhino Rangers ya Tabora, Milambo Camil alisema anakoshwa zaidi na namna mido hiyo inavyoitumikia vizuri nafasi yake nyuma ya washambuliaji na kuipa kazi nyepesi safu inayoongozwa na Fiston Mayele na Jesus Moloko.

Mbali na Fei, kocha huyo wa zamani wa Milambo na Singida United alimtaja pia straika wa Polisi Tanzania Vitalis Mayanga ambaye ni kinara wa mabao kwenye ligi akifunga manne katika mechi tano na anavutiwa na alivyorudi kwenye kiwango bora na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga.

“Nimevutiwa na wachezaji kama Fei Toto wa Yanga kwa namna anavyoitumikia vizuri nafasi ya kiungo nyuma ya mshambuliaji na Vitalis Mayanga aliyerudi katika kiwango bora na anavyojiweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga,” alisema.

“Muhimu kwao ni kudumisha nidhamu ya chakula na vinywaji, nidhamu ya maisha ya kiuchezaji na nidhamu ya mazoezi ili wawe na mwendelezo mzuri wasije wakaishia njiani ikaonekana ni nguvu ya soda tu,” alisema.

Related Azam yakamilisha raundi ya tatu kibabe Feisal ampa Zahera mchongo wa kuiua Simba Feitoto na unahodha Manara ashindwa kujizuia kwa FeitotoAkitoa tathmini yake kwenye mechi tano za kwanza aliliambia Mwanaspoti Ligi Kuu imekuja na moto mkali, timu zimejiandaa vizuri na kila mechi zimekuwa na ushindani zaidi, huku akivutiwa na namna timu karibu zote zinacheza mpira kwa mbinu.

Naye Katibu wa Panama FC ya Iringa, Enock Staki alisema bidii na kuzingatia maelekezo ya walimu wao ndicho kimefanya nyota hao wafanye vizuri, kuonekana na kukubalika na wengi huku wakichagizwa na vipaji vikubwa walivyonavyo.

“Ni vizuri kwao kutolewa sifa, waongeze bidii na wajitunze ili wafanye vizuri zaidi, waendelee pia kudumisha ushirikiano na wenzao na kuendelea kuwatii walimu wao ili wasije kuelemewa na sifa wakabweteka,” alisema Staki.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz