Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Samatta hajapenda mwanae na Msuva kutemwa Taifa Stars

Morocco X Msuva X Samatta Mzee Samatta hajapenda mwanae na Msuva kutemwa Taifa Stars

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba mzazi wa Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta ameonesha kutofurahishwa na kitendo cha Kocha wa Timu ya taifa ya Tanzania, Hemed Morocco kuwaacha nyota wa timu hiyo, Mbwana Samatta na Simon Msuva kuelekea michezo miwili wa kufuzu AFCON 2025 ambayo itafanyika hivi karibuni.

Morocco aliita kikosi cha wachezaji 23 jana ambao wataunda kikosi cha Stars kuelekea michezo hiyo huku akisema kuwa Samatta bado ni mchezaji wa Stars na atamtumia muda atakapomhitaji kulingana na mahitaji ya mchezo huku akiongeza kuwa amemuacha Msuva kwa sababu bado anashughulikia changamoto zake kuhusu timu anayotaka kujiunga nayo.

"Inaonekana kuna aina Fulani ya chuki kutokana na mafanikio ya mwanangu Mbwana, bado Mbwana ana nafasi kubwa sana katika timu ya taifa, Samatta na Msuva ni wachezaji muhimu sana kwenye taifa letu, kwa asilimia kubwa wao ndio wamesababisha tufuzu kucheza AFCON zote mbili

"Kwenye kombe la dunia 1966, Pele alipata majeraha dhidi ya Ureno lakini mechi iliyofuata alicheza kwa sababu alipigwa sindano ya ganzi na wakawa wanamuogopa sababu yupo nje; hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwa Samatta vivyo hivyo kwa Msuva

“Kocha Hemed Morocco amekosea sana kuwaacha Samatta na Simon Msuva,” amesema Mzee Ally Samatta Baba mzazi wa Mbwana Samatta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live