Mwanachama wa klabu ya Yanga, Mzee Mpili amesema hawamtaki tena kiungo wao Feisal Salam maarufu Fei Toto kurudi katika kikosi cha timu hiyo.
Akizungumza leo Machi 1 mbele ya Wanahabari Mzee Mpili ambae ni mpenzi wa Yanga kindaki ndaki amesema
"Asirudi tena Yanga mpaka tunamaliza Ligi au tunamaliza miaka yake (2024) mkataba wake utakapomalizika"
Feisal aliomba kuvunja Mkataba wake ndani ya Yanga, Huku uongozi ukikataa kuridhia ombi hilo wakidai ana mkataba mpaka Mei 30, 2024.
Msikilize kwa urefu zaidi Mzee mpili hapa chini;
#VIDEO Mwanachama wa klabu ya @yangasc1935 Mzee Mpili amesema hawamtaki tena kiungo wao @feisal194 kurudi katika kikosi cha timu hiyo.
— EastAfricaRadio (@earadiofm) March 1, 2023
Video kamili ipo youtube ya #EastAfricaRadio#MzeeMpili #Nabi #TFF #Michezo #YangaSC #FeiToto pic.twitter.com/II2PXllaH9