Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Mpili: Simba wanavaa magunia

MZEE MPILI 2345 Mzee Mpili

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki na mwanachama kindakindaki wa Yanga, Haji Omari maarufu kama Mzee Mpili amewatupia dongo watani zao wa jadi, Simba Sc kuwa hawana jezi zenye ubora kama za Wananchi.

Mzee Mpili ametoa dongo hilo leo Jumanne, januari 31, 2023 baada ya kupata jezi mpya ya Yanga iliyozinduliwa jana kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Nashukuru nimepata jezi yangu, hii ina ubora wa juu kuliko zile za mwanzo, inaokena hata kwa macho, inatisha. Nawasihi Wanayanga wenzangu waje kuchukua jezi tuzimalize ikiwezekana leo hii hii ili pesa isaidie kwenye matumizi mengine ya klabu.

“Ulinganisha na wenzetu, jezi za mtani (Simba Sc) ni magunia, sio jezi hizo ya kufikia ubora wa Young Africa, hii jezi ya Wananchi ni orijino, za kwao ni magunia tena manyang’unyang’u. Hawana hela ya kutengeneza jezi kama hizi.

“Kwanza hawana wadhamini, wangekuwa na hela wachukue wachezaji wa kuokotaokota? Hakuna mchezaji anayeeleweka pale, wengi wamepewa kwa mkopo. Yule Manzoki wamemleta juzi amesajiliwa China amekuja kupiga kura Simba, wamewatia ujinga wananchama wao, hawana akili,” amesema Mzee Mpili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live