Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Manara afunguka kuhusu Haji kutimka Simba

Video Archive
Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya Aliekua Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kueleza sababu za kung'atuka katika nafasi hiyo,hii leo baba yake mzazi na nyota wa zamani wa klabu ya Young Africans , Sunday Manara ametoa kauli yake kuhusu tukio hilo.

Mzee Sunday Manara ametoa kauli hiyo leo agosti 5,alipoulizwa na waandishi wa habari ana maoni gani baada ya Haji kuondoka Simba.

"mimi hainihusu,mimi ni yanga,kunapotokea migogoro kama hiyo ndani ya Simba mimi nafurahi, akitokea mwingine tena akaondoka ndio tunafurahi zaidi sisi yanga kwa sababu hayo ndiyo waliyotufanyia sisi kwa maana hiyo hili kwetu ni faraja"amesema Mzee manara.

Aidha alipoulizwa kama siku moja angependa Haji Manara aje kuwa msemaji wa Klabu ya Yanga alijibu,

"Wala hatumtaki,kwa sababu alishawahi kusema kuwa haipendi Yanga,abakie huko huko Simba kwake na ninajua inamuumiza sana kuondoka Simba kwa sababu ni kitu ambacho anakipenda sana maishani mwake lakini hayo ni maamuzi yake kwa kuwa ni mtu mzima" alisisitza Mzee Manara

Sunday Manara maarufu kama "computer" alipata kuichezea Klabu ya Yanga ambayo ni Mpinzani wa Jadi wa Simba na mwanae Haji Manara ni Shabiki Mkubwa wa Klabu ya Simba na kufikia kuhudumu nafasi ya Usemaji katika klabu hiyo kwa miaka isiyopungua 6 mpaka alipong'atuka siku chache zilizopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live