Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Magoma kuilipa Yanga sh milioni 100, akishindwa kifungo kinamfuata

Mzee Magoma 713.jpeg Mzee Magoma kuilipa Yanga sh milioni 100, akishindwa kifungo kinamfuata

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Agosti 9, 2024, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Juma Magoma na wenzake, yaliyolenga kuundoa uongozi wa Klabu ya Yanga madarakani na kuweka kando tuzo na amri zote zilizotolewa katika hukumu iliyowapa ushindi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga, alitoa uamuzi huo wakati wa kusikiliza marejeo ya shauri la maombi namba 187/2022, yaliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Katika uamuzi huo, Mahakama imekubaliana na madai ya Bodi hiyo kwamba wazee hao hawakuwa na sifa za kisheria za kufungua shauri hilo.

Zaidi ya hayo, Mahakama imeamuru Magoma, Geofrey Mwaipopo, na Abeid Mohamed Abeid kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo kwa Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Uamuzi huu unaweka mwisho kwa jaribio la kuondoa uongozi wa klabu hiyo, huku Bodi ya Wadhamini ikipata ushindi katika shauri hilo.

Mzee Magoma na wenzake walishinda kesi waliyokuwa wamefungua mahakamni hapo wakipinga uhalali wa Baraza la Wadhamini la Yanga.

“Hukumu hiyo imefuta na kwa vile Yanga imetumia gharama kuja hapa mahakamani, kutafuta wanasheria wa kutuaidia, mimi mwenyewe natakiwa nilipwe, nilikuwa na mawakili wengine wa Yanga, mama Karume alikuwa na wakili wake, mzee Katundu alikuwa na wakili wake, hivyo Mzee Magoma na wenzake wamemariwa kutulipa gharama za usumbufu ambazo tukikaa tukapiga hesabu vizuri zitakuwa kama tsh milioni 70 mpaka sh milioni 100.

“Mashabiki waendelee kuisapoti timu yao, ile sintofahamu ya kina mzee magoma na wenzake imefutwa rasmi leo na hawana chao tena. Sisi kwa upande wetu tumemaliza hapa kinachofuata ni kufungua kesi kudai fidia ya gharama zetu ambazo tumezitumia.

“Ni haki yao kukata rufaa lakini sheria namba 318 inasema masuala yote yanayohoji uhalali wa baraza la wadhamini yanatakiwa yapelekwe mahakama kuu, sasa wewe umepeleka mahakama ya Kisutu na Mahakama ya Kisutu imejiridhisha kuwa haikupaswa kusikiliza kesi hiyo, sasa wewe unakata rufaa kwenda wapi? Wakikata rufaa watapoteza muda ila popote waende tutawafuata.

“Unaposema gharama lazima udhithibitishe, tukikamilisha tutakwenda mahakamani kuzidai na wakishaamua mahakama kwamba anatakiwa alipe kiasi gani basi ni lazima azilipe ndani ya siku 60, akishindwa kulipa sisi kama yanga SC tutakwenda kukamata mali zake ili kufidia gharama zetu, na ikithibitika hana mali ambazo zinaweza kukidhi gharama zetu basi tutamuomba awe mfungwa “Civil Prison” mpaka atakapomaliza kulipa madeni yetu," amesema Wakili Simon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live