Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Kamwe: Bora nipigwe risasi kuliko kuishabikia Yanga

Kamwe Bababa Mzee Kamwe: Bora nipigwe risasi kuliko kuishabikia Yanga

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba Mzazi wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabuya Yanga, Ally Kamwe amekanusha kauli ya mtoto wake kusema amehama na Clatous Chama aliyehamia Yanga SC.

Mwanzoni mwa wiki hii Ali kamwe akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa baba yake amehama Simba na kumfuata Chama Yanga SC.

“Sijawahi kuwa na mawazo ya kuishabikia Yanga, sifikirii wala sitofikiria, ikiwekwa risasi na Yanga nachagua risasi. Niko tayari kufa lakini sio kulazimishwa kuishabikia Yanga.

“Kamwe anahitaji utani na baba yake na ndiyo utani wa mpira ulivyo, utani wa mpira hauhitaji hasira kama utataniwa utani kama huu ukasirike na ukamtania mwenzako kesho akacheka, ujue utani wa mpira sio ugomvi bali utani.

“Sijawahi kuwa Mwanayanga hata siku moja, bora nichague risasi badala ya kuishabikia Yanga,” amesema Mzee Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live