Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Dalali: Nilianzisha Simba Day nipate pesa ya kulipa madeni

Hassan Dalali Mzee Dalali

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Hassan Dalali amefunguka kwa uwazi sababu za kuasisi Tamasha la Simba (Simba Day) ambalo kwa mwaka huu 2023 limefanyika jana Agosti 6, 2023 kwa mara ya 15 mfululizo tangu kuasisiswa kwake mwaka 2009.

Dalali chini ya Uongozi wake, Dalali aliasisi Tamasha la Simba Day kama sehemu ya kuiwezesha klabu hiyo kupata fedha za kujenga uwanja wake wa mazoezi maeneo ya Bunju, ambapo kwa sasa Uwanja huo unaitwa Mo Simba Arena ambao ndio unatumika kwa mazoezi ya kikosi cha Simba SC kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu na Michuano ya kimataifa.

Dalali amesema anaamini mchango wake ndani ya klabu ya Simba utaendelea kuenziwa na amewataka Mashabiki na Wanachama kuendelea kulidumisha Tamasha la Simba (Sima Day) ambalo kila mwaka limekua likiimarika kwa kuongezewa mambo mazuri.

"Nimefurahi sana na ninawapongeza viongozi kwa jinsi ambavyo wameendeleza hili jambo, ni jambo zuri, ni jambo kubwa sasa hivi limeshavuka Afrika liko Ulaya, nadhani mwakani Liverpool au Manchester United wanaweza wakafanya tamasha kama hili.

"Wakati naanzisha miaka ile, sikutegemea kama Tamasha litakuwa kubwa kiasi hiki. Tulianzisha hii kwa ajili ya kupata pesa ya kulipa deni la uwanja wa Bunju sababu niliutafuta mimi pia.

"Simba ni timu kubwa, ina wapenzi wengi kuliko Yanga tangu zamani, leo imejidhihidirsha na watu wameona. Mashabiki wa Simba wanaipenda timu yao ni watu wa mpira.

"Baada ya hapa tunaelekea Tanga kwenye michuano ya Ngao ya Jamii, ninaamini tutafanya vizuri," amesema Mzee Dalali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live