Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzamiru hamfikii Kanoute, Simba watafute mkabaji - Mchambuzi

Kanoute, Ngoma Mzamiru Mzamiru hamfikii Kanoute, Simba watafute mkabaji - Mchambuzi

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa, eneo ambalo Simba wanapaswa kuliboresha ni kiungo mkabaji.

Wakanda amesema kuwa makocha ambao wamepita Simba hivi karibuni walikuwa wakimtumia Sadio Kanoute kama kiungo mkabaji lakini kiasili sio nafasi yake.

Simba tayari wameshamsajili kiungo mkabaji, Babacar Sarr raia wa Senegal kama mchezaji huru akitokea US Monastir ya Tunisia baada ya kumaliza mkataba wake.

"Simba hivi sasa eneo ambalo mimi naona ni muhimu sana na ambalo wanahitaji kulifanyia maboresho ni eneo la kiungo mkabaji. Hii position ndiyo imewahukumu Simba kwenye michezo mingi sana, ni eneo ambalo Robertinho ame-struggle sana akijaribu ku-switch wachezaji lakini haikuonekana kupata suluhisho.

"Sasa hivi amekuja Benchikha ambaye angalu sasa hivi tunamuona anamtumia Sadio Kanoute pamoja na Fabrice Ngoma, lakini kiungo mkabaji wake ambaye ni Primary ni Sadio Kanoute, muda ambao anakosekana Kanoute akiingia Mzamiru, Mzamiru hakupi kile ambacho Kanoute huwa anakupa," amesema Wakanda Republic.

Wachezaji wa Kigeni Simba mpaka sasa ni 13 hivyo wanatakiwa kupunguza mchezi mmoja wa kimataifa ili kukidhi kanuni;

Willy Onana

Moses Phiri

Clatous Chama

Luis Miquissone

Sadio Kanoute

Fabrice Ngoma

Ayoub Lakred

Henock Inonga

Che Malone

Jean Baleke

Aubin Kramo

Saido Ntibazonkiza

Babacar Sarr - Usajili mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live