Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzamiru Yassin pumzi ya kikosi cha Simba jana na leo

Mzamiru Goal.jpeg Mzamiru Yassin pumzi ya kikosi cha Simba jana na leo

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zipo hadithi nyingi kuhusu Claude Makelele, Ni yule Mzaliwa na Kinshasa pale DR Congo. Yule mwanaume aliyekuja duniani kutuonyesha namna ya kumiliki dimba la chini.

Kwenye ile Real Madrid Galacticos ya mwaka 200-2003. Real Madrid ya Zinedine Zidane,Ronaldo De Lima,Luis Figo,Raul Gonzalez.

Claude Makelele alikuwa mtu pekee aliyekubali kubeba mateso ya Real Madrid alikaba na kulinda wanaume wa nne nyuma yake. Alikuwa maana halisi ya kiungo mkabaji.

Aliwapa kila kitu Real Madrid likiwamo taji la Ulaya 2002. Aliondoka kuupisha usajili wa David Beckham. Kilichowakuta Madrid waliishi misimu mitatu bila ladha ya ubingwa.

Mnaikumbua Makelele Role? Baada tu ya kutua EPL pale Darajani. Wakina Lampard,Drogba,Arjen Robben walinufaika na jasho la Claude Makelele.

Zipo hadithi kuhusu Roy Kean na Manchester United,Zipo hadithi kuhusu Marco Senna. Zipo hadithi kuhusu Clarence Seedorf na Ac Milan tishio wakati ule.

Kwenye ardhi ya Mwalimu Julius Nyerere zipo hadithi kuhusu uzao wa kiungo chuma. Mzamiru Yassin ambaye anaishi kwenye dunia yake mwenyewe.

Dunia ambayo hasifiwi sana, Haimbwi sana, Lakini ameamua kuishi hivyo sio mtu wa Camera sana anachojua ni kumikili eneo la kati tu.

Wakati wazungu wanasema NGOLO KANTE IS everywhere, Ndani ya kikosi cha Simba wanae Mzamiru Yassin.

Atakata umeme kwa energy ile ile ndani ya dakika 90. Uwezo mkubwa wa kulinda safu ya ulinzi. Na namna ambayo anaisogeza timu kutoka chini.

Sifa nyingine ni namna ambavyo anaongeza nguvu kwenye final third, Uwezo wa kukanyaga kila jani la uwanja. Mitaa inamuita kiungo punda, Mapafu imara sana.

Ni mtu muhimu sana ambaye amelizika kuishi dunia yake. Hawezi kufanya Locomotive feints za Clatous Chama, Hawezi kufunga kama Jean Baleke.

Lakini yeye ni pumzi ya kikosi cha Simba, Mzmiru Yassin ni wa jana na leo kwenye dunia yake ambayo ameamua kuishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: