Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzambia apiga goli 4 Ulaya

Daka Mshambuliaji wa Leicester, Patson Daka

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Patson Daka, usiku wa Jumatano amefunga mabao yote manne kuiwezesha Leicester City kushinda 4-3 dhidi ya wenyeji, Spartak Moscow katika mchezo wa Kundi C michuano ya Uropa Ligi Uwanja wa Otkrytiye Arena Jijiji Moscow, Urusi.

Daka mwenye umri wa miaka 23 alifunga mabao hayo dakika za 45,48, 54 na 78, wakati mabao ya Spartak Moscow yalifungwa na Aleksandr Sobolev dakika ya 11 na 86 na Carl Henrik Jordan Larsson dakika ya 44.

Kwa matokeo hayo, Leicester City inafikisha pointi nne na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Legia Warsaw baada ya mechi tatu za awali.

Spartak Moscow inabaki nafasi ya tatu na pointi zake tatu mbele ya Napoli yenye pointi moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live