Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwisho wa ligi, usalama ni muhimu sana

Ligi Kuu Pic Mwisho wa ligi, usalama ni muhimu sana

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Haitakuwa mwisho mpa¬ka ifike mwisho kwenye mashindano yote ambayo timu zinashiriki iwe ni kwenye ligi ama Kombe la Shirikisho.

Kwa sasa tunaona kuna timu ambazo zimeshatambua wapi zitakuwa msimu ujao lakini kuna mechi ambazo wanazo mkononi hizi zinawahusu la¬zima wacheza.

Zipo pia ambazo zina mechi kwenye Kombe la Shirikisho ikiwa ni hatua ya nusu fain¬ali hakika kazi bado ni ngumu kwenye dakika 90 za kusaka ushindi.

Ambacho kinatakiwa ni uma¬kini na maandalizi mazuri kwe¬nye mechi zote bila kujali aina ya mashindano husika.

Muhimu ni kupata matokeo baada ya dakika 90 na haya hayajitokezi bure ni lazima ku¬pambana bila kuchoka na ku¬fanya maandalizi mazuri.

Msingi mkubwa unajengwa kwenye nidhamu nje na ndani ya uwanja na hili litawafanya wachezaji kuonyesha upekee wao kwenye kukamilisha safari ya mwisho.

Hakuna ambaye hapendi kuona timu inapata matokeo lakini kikubwa ni kujipanga kwa umakini nakutumia nafasi ambazo zinapatikana kwenye mechi husika.

Mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa ambacho kinahita¬jika kwa timu ambayo inahitaji ushindi ni kuwa makini kwe¬nye kupunguza makosa.

Jambo lingine muhimu ni afya za wachezaji kwa kulindana ndani ya uwanja wakati huu wa ligi kugota mwisho.

Imekuwa ni kasumba ya wachezaji wengi kupenda ku¬tumia nguvu kubwa wakati huu wa lala salama hii sio sawa ni muhimu kila mchezaji kuwa makini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: