Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwinyi Zahera kuanza kazi rasmi leo

Mwinyi Zahera Namungo Mwinyi Zahera kuanza kazi rasmi leo

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tabora United baada ya kupoteza mchezo wao wa nyumbani kwa kipigo kizito 4-0 kutoka kwa Simba, leo watakuwa nyumbani tena uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kutafuta alama tatu dhidi ya Namungo FC.

Tabora United ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 15 wakati Namungo yenyewe ipo nafasi ya nane ikiwa na alama 17.

Mchezo huu utakuwa ni wa kwanza kwa Kocha Mwinyi Zahera ambaye atakuwa anarejea tena uwanjani akiwa na Namungo FC tangu alipoachana na Coastal Union ya Tanga.

Mwinyi Zahera tangu alipoondoka Yanga hakuna mahali ambapo alifanikiwa wala kudumu kwa muda mrefu kwa timu alizozifundisha [Gwambina FC, Polisi Tanzania, Coastal Union na sasa Namungo FCJ.

Tusubiri kuona kile ambacho Papaa Mwinyi Zahera atakifanya ndani ya 'Southern Killers' kama itakuwa ni tofauti na alichofanya kwenye baadhi ya klabu alizofundisha hivi karibuni.

TABORA UNITED V/s NAMUNGO UWANJA WA ALI HASSAN MWINYI, TABORA SAA 8:00 MCHANA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live