Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwinyi Zahera awasilisha barua ya utetezi

Mwinyi Zahera Atimuliwa Kocha Mwinyi Zahera

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mwinyi Zahera amewasilisha barua rasmi ndani ya uongozi wa wa Coastal Union, kuelezea sababu ya kikosi hicho kuanza vibaya msimu huu na hii ni kutokana na uwepo wa taarifa zinazomuhusu kuzuiwa kujiunga na kambi.

Hilo linajiri baada ya viongozi wa klabu hiyo kumzuia kujiunga na kambi ya timu iliyokuwa jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya lhefu utakaopig wa Jumamosi hii ya Oktoba 21, kwenye Uwanja wa Highlands Estate.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Abbas Elsabri amesema hawezi kuweka wazi juu ya taarifa hizo hadi pale atakapopata ukweli kutoka kwa viongozi ambao ndio wana jukumu kubwa la kumpatia ili aweze kuzitoa kwa umma.

“Kama zipo basi sisi tutaweka wazi ila kwa sasa tambua tu kwamba tunaendelea na maandalizi yetu kwa ajili ya mchezo na lhefu, lengo ni kupata matokeo mazuri kwa sababu ukiangalia tulivyoanza msimu ni tofauti na malengo yetu, amesema.

Wakati Elsabri akizungumza hayo imefahamika kuwa Zahera amewasilisha barua ya kueleza kwa nini tịmu hiyo haina matokeo mazuri tangu msimu umeanza kutokana na kucheza michezo mitano ya Ligi Kuu Bara bila ya kupata ushindi wowote.

Wakati Zahera amewasilisha ripoti yake imetambulika kuwa, kwa sasa kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Fikiri Elias huku viongozi wakimuongezea nguvu nà staa wa zamani wa klabu hiyo akiwemo, Razak Yusuf maarufu ‘Careca.

Katika michezo mitano aliyoiongoza kikosi hicho Zahera ametoa sare miwili na kupoteza mitatu huku timu ikiwa mkiani na pointi zake mbili tu.

Chanzo: Dar24