Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwinyi Zahera: Miaka miwili ijayo Mzize hatacheza tena Afrika

Mwinyi Zahera F583f0d835.jpeg Mwinyi Zahera: Miaka miwili ijayo Mzize hatacheza tena Afrika

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga ambaye kwa sasa ni kocha wa Namungo Mwinyi Zahera akizungumza na kituo cha habari cha AzamTv kuhusu Mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize amesema kuwa Nyota huyo miaka miwili ijayo hawezi kucheza mpira Afrika.

Kocha huyo amedai kuwa Clement Mzize amekuwa ni kinda hatari na mabadiliko yake yamekuwa ni makubwa kila siku na yeye alishamtabilia makubwa huko nyuma huku akiendelea kusisitiza kuwa Mzize lazima akacheze ulaye kwasababu ya Uwezo wake.

kauli hiyo ya Zahera ambaye ndiye alikibaini kipaji cha Mzize na kumleta Yanga ya vijana kabla ya kupandishwa kwenda timu kubwa, amesema hayo huku kukiwa na tetesi nyingi kuhusu mchezaji huyo kutakiwa na timu kubwa Barani Afrika kama Wydad AC na Kaizer Chiefs.

Tangu apandishwe kutoka Yanga (B)

Season 21|22

⚽ 07 Assist 02 - Top scorer ligi ya vijana (U-20)

Season 22|23 :

Tuzo ya Mchezaji bora chipukizi.

⚽ 05 Assist 03 - Ligi kuu Tanzania bara.

⚽ 05 Assist 01 - FA cup.

⚽ 10 Assist 04 - Total.

Season 23 | 24 :

⚽ 06 Assist 07 - Ligi kuu Tanzania bara.

⚽ 03 Assist 01 - (CAF) champions league.

⚽ 05 ????️ 02 - (FA) cup top scorer.

⚽ 14 Assist 10 - Total.

Season 24 | 25

Mechi tatu, Magoli mawili.

Key

______

⚽ - Magoli.

Takwimu, mashindano rasmi pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live