Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwinyi Zahera: Ligi bado, mbona kitaeleweka tu

Zahera Pic Papaaaa Mwinyi Zahera: Ligi bado, mbona kitaeleweka tu

Fri, 10 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amewatoa hofu mabosi wa timu hiyo kwamba atainusuru timu isishuke daraja na msimu ujao itacheza Ligi Kuu.

Polisi Tanzania kesho Ijumaa, inatarajia kutua Dodoma kwaajili ya mchezo wa Ligi utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri dhidi ya Dodoma Jiji ambayo nayo ipo kwenye hali tete.

Zahera alitangazwa kocha mkuu akichukua nafasi ya Joslin Sharif, aliyetimuliwa Oktoba 17 sambamba na msaidizi wake, Augustino Damian na timu kuwa chini ya John Tamba ambaye awali alikuwa kocha wa viungo.

Tangu Desemba 2, alipotangazwa kuwa kocha mkuu timu hiyo imecheza michezo 10 akishinda michezo miwili, ilipoichapa mabao 2-0 Namungo kisha ikaifunga Tanzania Prisons bao 1-0, sare nne na kuchapwa michezo minne.

Afisa Habari wa timu hiyo, Frank Lukwaro alisema Zahera amewahakikishia kupambana ili kukwepa kushuka daraja kwani wanashika nafasi ya 15 kwa alama 19. "Kitu kikubwa ambacho kocha alisema kuna tatizo eneo la ushambuliaji ambapo nafasi nyingi zilizokuwa zikipatikana zilikua hazizai matunda mazuri.

"Baada ya wiki mbili kukaa bila mchezo ameyafanyia kazi mapungufu hayo na kuahidi matokeo mazuri katika michezo inayofuata tukianza na Dodoma Jiji wiki hii," alisema Lukwaro.

Aliongeza bado hawajakata tamaa na matumaini ya kubaki Ligi Kuu ipo sababu michezo iliyobaki inaweza ikawafanya kupanda nafasi za juu kama watapata matokeo mazuri.

Lukwaro alisema uongozi wa timu unapambana kuona wanakamilisha stahiki zote za wachezaji na benchi la ufundi ili wachezaji wanatimiza vyema majukumu yao uwanjani.

Baada ya mchezo huo Polisi itakuwa imesalia na michezo mitano dhidi ya Singida, Ihefu, Mtibwa, Simba kisha itamaliza msimu kwa kucheza na Azam.

Polisi Tanzania ilipanda Ligi Kuu msimu wa mwaka 2019/20 pamoja na Namungo FC ikiwa chini ya Mbwana Makata ambaye baada ya hapo alikwenda kuipandisha Dodoma Jiji (2020/21).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live