Mwili wa mwanasoka Christian Atsu, aliyefariki katika tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki wiki mbili zilizopita, umerudishwa nchini kwao Ghana.
Ndege iliyobeba mwili wa marehemu ilitua mjini Accra Jumapili jioni, na jeneza lake lilibebwa na wanajeshi wa Ghana.
Atsu alikutwa amefariki siku ya Jumamosi chini ya nyumba yake kusini mwa Uturuki.
Alikuwa akiichezea klabu ya Hatayspor.
Winga huyo aliichezea timu ya taifa ya Ghana mara 65 na kuisaidia timu yake kufika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alichezea timu za Premier League Everton na Newcastle.
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Kotoka katika mji mkuu wa Accra, Makamu wa Rais wa Ghana Mahamudu Bawmia alisema:
"Tulikuwa na matumaini dhidi ya matumaini, kila siku iliyopita, tulisali na kuomba.
Lakini alipopatikana akiwa amefariki." Bw Bawmia aliongeza kuwa mwanasoka huyo alipendwa sana na atakumbukwa sana.
"Ni maumivu makali mno kumpoteza." Na kuahidi kuwa Atsu atapewa mazishi "ya heshima"