Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa Gamondi upo Dar, akili ipo Ethiopia

Gamondi Chama Dube Abuya 91021 Mwili wa Gamondi upo Dar, akili ipo Ethiopia

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi mwili wake upo Dar es Salaam, lakini akili ipo Addis Ababa, Ethiopia kwenye mechi ya marudiano ya CBE ya huko na SC Villa ya Uganda. Mshindi wa mechi hiyo atacheza na Yanga inayohitaji japo sare yoyote kusonga mbele.

Villa ililala mabao 1-2 nyumbani. Endapo Yanga itafuzu na kukutana na mshindi kati ya CBE au Vila, mabingwa hao wa soka Tanzania wataanzia ugenini kati ya Septemba 13-15 kisha kurudiana hapa nchini kati ya Septemba 20-22.

Gamondi ameangalia rekodi za Yanga dhidi ya timu za Ethiopia akaamua kujiongeza na kutuma watu haraka ambao wikiendi hii watakuwa jukwaani wakiangalia mechi hiyo. Rekodi zinaonyesha kwenye michuano ya CAF Yanga haijawahi kushinda Ethiopia.

Kati ya Kocha wao msaidizi Mussa Nd’ew au mtaalam wa kuwasoma wapinzani, Msauzi Mpho Maruping, mmoja wao ataongoza msafara wa watu wawili kwenye kuisoma CBE ambao taarifa zao za awali imepenyezewa wanacheza soka la pasi nyingi na kasi, hatua ambayo wanataka kuwajua haraka kabla ya kukutana nao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live