Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa zamani wa Yanga Madega afariki dunia, kuzikwa kesho

Imani Madega .jpeg Mwenyekiti wa zamani wa Yanga Madega afariki dunia, kuzikwa kesho

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Wilaya ya Chalinze, Musoga.

Kifo cha Mwenyekiti huyo kimethibitishwa leo Jumamosi Februari 10, 2024 na mwanaye, Abdul Madega alipozungumza na Mwananchi kwa simu.

Amesema baba yake alimpigia simu asubuhi na kumweleza kuwa anajisikia vibaya na kumwambia ampeleke Hospital ya Wilaya ya Chalinze, Musoga.

"Leo asubuhi mzee alinipigia simu kuniambia anajisikia vibaya nimpeleke hospitali, nikafika nyumbani, lakini alikuwa anatembea na nguvu zake kabisa, tukafika hospitali akaanza kutibiwa maradhi ya presha," "Akawa anaendelea vizuri tu, baada ya kufika saa tano asubuhi, akaaga dunia,” amesema Abdul.

Madega anatarajiwa kuzikwa kesho saa 10:00 jioni nyumbani kwake Chalinze mkoani Pwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live