Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti Kitayose FC atuhumiwa kwa Rushwa

Kitayoseeeee Kikosi cha Kitayose FC

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Fountain Gate FC, imemripoti kwenye Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mwenyekiti wa timu ya Kitayosce FC, YUSUPH KITUMBO, kwa tuhuma za kuwarubuni wachezaji wao ili kucheza chini ya kiwango katika mchezo wa Ligi ya championship iliyozikutanisha timu hizo Jana Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Shabiby mjini Gairo ambao ulimalizika kwa timu hizo bila kufungana.

Kwa mujibu wa WENDO MAKAU ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, amesema Mwenyekiti huyo alituma pesa kiasi cha Tsh. Milioni 2 na zaidi kwa Wachezaji zaidi ya watano wa nafasi mbalimbali Ili wagawane kiasi hicho cha fedha.

Wachezaji hao waliripoti suala hilo Kwa uongozi wao ndipo uongozi wa Fountain ukaripoti Takukuru na jana kabla ya mchezo na Mwenyekiti huyo wa Kitayosce FC alihojiwa Takukuru na kuacha baadhi ya simu zake kwa hatua zaidi za kiuchunguzi.

Jumanne ya wiki inayoanza Kesho, uongozi wa Fountain Gate utaripoti suala hilo kwenye shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

Alipotafutwa Kwa nyakati tofauti Mwenyekiti huyo ili kupata kauli yake juu ya suala hilo, simu yake haikupatikana hewani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live