Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwendo wa Panga la pointi Championship

Reading Klabu ya Reading yakumbana na adhabu Championship, yakatwa alama sita

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Reading nayo imekatwa pointi sita kwa kuvunja sheria ya matumizi ya fedha zilizowekwa na shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza.

Reading inakuwa klabu ya pili kukubali na kukatwa pointi hizo baada ya Derby County na yenyewe kukatwa pointi 21 kutokana na kuvunja kanuni za mapato na matumizi ya fedha.

Klabu ya Reading imekubali kupunguzwa pointi hizo na wametoa waraka unaosema kuwa wanakubaliana na maamuzi na hawana mpango wa kukataa rufaa, huku mmiliki wa klabu hiyo akisema ameyapokea maamuzi hayo na bado atajitolea kwa klabu kwa moyo wake wote.

Kwasasa wanashuka kutoka nafasi 16 mpaka ya 19 kwenye msimamo wa ligi ya Championship wakiwa juu ya Derby County kwa nafasi nne kwa timu zinazopigania kutoshuka daraja huku Derby akiubeba msimo wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live